Nafasi za Kujiunga na Chuo Mwaka wa Masomo 2025-2026
- May 19, 2025
- Bucohas
- 0
MKUU WA CHUO CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI BUMBULI KILICHOPO MKOA WA TANGA WILAYA YA LUSHOTO HALMASHAURI YA BUMBULI ANAWAKARIBISHA WANAFUNZI WOTE WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE AU CHA SITA, WENYE SIFA ZA KUJIUNGA NA TAALUMA ZA AFYA KWA KOZI ZIFUATAZO.
➡ORDINARY DIPLOMA IN MEDICAL LABORATORY SCIENCE (Stashahada ya Maabara) Sifa za mwombaji mwanafunzi awe na ufaulu wa kuanzia alama D katika masomo manne yakiwemo Biology, Chemistry, Mathematics au Physics au Engineering Sciences au ufaulu zaidi ya huo.
➡ORDINARY DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE (Stashahada ya Utabibu) Sifa za mwombaji ufaulu wa kuanzia alama D katika masomo manne yakiwemo Biology, Chemistry na Physics/Engineering Sciences ) au ufaulu zaidi ya huo.
➡WANAOJIENDELEZA (UPGRADERS) IN CLINICAL MEDICINE:- Sifa ya mwombaji awe mhitimu ya ngazi ya Astashahada ya Utabibu (NTA LEVEL 5) kutoka Chuo kilicho sajiliwa na NACTVET.
➡WANAOJIENDELEZA (UPGRADERS) IN MEDICAL LABORATORY SCIENCE:- Sifa ya mwombaji awe mhitimu ya ngazi ya Astashahada ya Maabara (NTA LEVEL 5) kutoka Chuo kilicho sajiliwa na NACTVET
➡ PIA TUNATOA KOZI FUPI ZA KOMPYUTA
Sifa za mwombaji awe amemaliza elimu ya darasa la saba na anajua kusoma na kuandika.
➡ Chuo kimesajiliwa (NACTVET) kwa namba ya usajili: REG/HAS/073
➡ Chuo kina Hospitali ya kujifunzia
➡ Ada zetu ni nafuu na zinalipwa kwa awamu tatu
➡ Chuo kinatoa huduma ya hostel bure kwa wanafunzi wote
kinamazingira tulivu na mazuri kwa kujifunzia, Maktaba nzuri, Maabara ya kisasa na Chuo chetu kina walimu wazuri na wenye uzoefu wa muda mrefu katika kutoa mafunzo bora
Tangazo hili limetolewa na Dkt. Amani Simoni Lwoga Mkuu wa Chuo
